Monday, December 31, 2012

WATANZANIA WAZALIANA KWA KASI.
TANZANIA BARA"IDADI YA WATU" 43,625,434.

Tanzania Zanzibar "IDADI YA WATU" 1,303,568..

Leo tarehe 31/12/2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndug. Jakaya M. Kikwete atangaza rasmi idadi ya Watanzania kama ifuatavyo:

(01). Tanzania Bara "IDADI YA WATU" ni:- 43,625,434.
(02). Tanzania Zanzibar "IDADI YA WATU" ni:- 1,303,568.


Jumla ya Watanzania Bara na Watanzania Zanzibar ni: - 44,929,002.

Sunday, December 30, 2012

Dear our customers, 

Tunaendelea kuwaletea na kuwatengenezea bidhaa zenye ubora wa kitaifa na kimataifa   "FBC - Sharing Happiness", Tafadhali endelea kutumia bidhaa zetu popote utakapozipata Tanzania na ujionee ladha taaaam, na hivi karibuni tutawaletea bidhaa mpya kabisa ndani ya soko. 
Asanteni sana - Buy Tanzanian Products. 
Merry Christmas & Happy New year 2013.








Friday, December 28, 2012

Kenya:
Madereva "WANAWAKE" wa pikipiki maarufu kama "Bodaboda" washamiri kwa wingi nchini kenye.

Mwanamke wa kizungu anyongwa mpaka kufa hotelini Dar.



 Raia  wa Bulgaria, Rola Cheterolia (42), mfanyakazi wa casino ya Kilimanjaro inayomilikiwa na Hoteli ya kitalii ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam, amenyongwa na watu wasiojulikana.

Mwili wa mwanamke huyo ulikutwa katika nyumba za kupanga zilizoko eneo la hoteli hiyo ya kitalii iliyoko Masaki.

Habari zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mwanamke huyo alinyongwa huku akiwa amefungwa mikono na miguu kwa kutumia kamba.

Marehemu alikuwa mfanyakazi wa casino hiyo na alikutwa na mkasa huo saa 3:00 usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku.

“Tunasikitika sana kwa kitendo hiki kilichofanywa na watu hawa wasiojulikana cha huyu mwanamke wa kigeni kuuawa huko Sea Cliff, lakini bado tunafuatilia kwa kina kwani upelelezi unaendelea kubaini waliohusika katika tukio hilo,” alisema Kamanda Kenyela.

Kamanda Kenyela alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kwamba hakukuwa na dalili zozote za uvamizi ama ujambazi.

Hata hivyo, alisema kuna uwezekano wa tukio hilo kuwa la ulipizaji kisasi, lakini alisisitiza kuwa upepelezi bado unaendelea.

Alisema mlinzi wa eneo hilo alikimbia baada ya tukio hilo na Jeshi la Polisi linaendendelea kumsaka.

Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff ulipoulizwa jana kuhusiana na tukio hilo, ulithibitisha kutokea na kusema kwamba marehemu aliuawa juzi usiku.


Hata hivyo, uongozi wa hoteli hiyo haukutaka kueleza zaidi na kusema kwamba suala hilo wamelikabidhi kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

“Ni kweli tukio hili limetokea pale `apartments' za Sea Cliff, na uchunguzi zaidi unaendelea, sisi hatuna cha kusema zaidi ya kukiri kwamba Rola ameuwa,” alisema mmoja wa watendaji waandamizi wa hoteli hiyo ambaye hata hivyo, hakutaka kutaja jina lake.

Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela, mwili wa marehemu Rola umehifadhiwa katika Hospitali ya Hindu Mandal.

Wakati huo huo, Kamanda Kenyela alisema mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake, ameuawa na wananchi wenye hasira wakati akijaribu kuiba pikipiki.

Kamanda Kenyela alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Magomeni Makuti wilayani Kinondoni na kukemea kitendo hicho cha wananchi kujichukulia sheria mikononi.

Na katika hatua nyingine, Kamanda Kenyela alitoa ufafanuzi kuhusu tukio la kuibwa kwa mtoto mwenye umri wa siku 21.
Aliwataka wazazi kujifunza kupitia tukio hilo na wasimuamini mtu yeyote na kuwakabidhi watoto wao.

Alisema upelelezi unaendelea na kutoa rai kwa wananchi iwapo watamuona mtu yeyote akiwa na mtoto asiye wake, watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mwenge baada ya mama wa mtoto huyo kumuomba mwanamke asiyefahamika amshikie mwanawe.

chanzo:nipashe

Thursday, December 27, 2012


DEAR OUR LOVELY CUSTOMERS,
THIS IS OUR NEW COMPANY "LOGO"
MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2013.

Monday, December 24, 2012

MAAFANDE WA KIBONGO HAPO MPO, JAMAA YUKO GWARIDE HAPO, HUKU AKISAGA "GOMBA" A.K.A MIADARATI, MIJANI, MIANDRAX.....
sawa sawa afande.........



SONG : Amazing Grace..

Amazing grace How sweet the sound , That saved a wretch like me , I once was lost, but now I'm found , Was blind but now I see, Twas grace that taught my heart to fear ,  And grace my fears relieved , How precious did that grace appear, The hour I first believed , My chains are gone, I've been set free, My God my Savior has ransomed me, And like a flood, His mercy reigns, Unending love, Amazing grace, The Lord has promised good to me, His word my hope secures, He will my shield and portion be As long as life endures, My chains are gone, I've been set free, My God my Savior has ransomed me, And like a flood, His mercy reigns,  Unending love, Amazing grace, My chains are gone, I've been set free, My God my savior has ransomed me, And like a flood, His mercy reigns, Unending love, Amazing grace, The Earth shall soon disolve like snow , The sun forbear to shine, But God, who called me here below, Will be forever mine, will be forever mine, You are forever mine.
MARRY X-MAS, HAKIKA MTOTO "YESU" KAZALIWA LEO TAREHE 25/12/2012.

The CEO of "FBC - Sharing Happiness" A Kibo Media Group and all stuff, wishes u a Merry Christmas & a Happy new year 2013.



Sunday, December 23, 2012

Ajali nje kidogo ya mji wa Chalinze

Basi limepata ajali nje kidogo ya mji wa Chalinze. Hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha,  ila wapo majeruhi. Basi lilikuwa linatokea Pangani Tanga kwenda Dar es Salaam'





Michezo:  Tanzania yaifunga Zambia 1-0

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeilaza timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo kwa bao moja kwa bila katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.



Katika mechi hiyo bao pekee la washindi, lilipatikana sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza likitiwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa.
Kwa upande wa timu ya Tanzania, ambao walionekana kutojiamini katika kipindi hicho, taratibu walibadilika, na kumiliki sehemu ya kiungo.
Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto,Frank Domayo na Salum Abubakar waliichosha ngome ya Zambia kwa kuelekeza mashambulizi mengi, langoni mwa Chipolopolo.
Mrisho Ngassa kama angekuwa makini zaidi angeweza kuipatia timu yake bao la mapema zaidi.
Timu ya Zambia ilichezesha nyota wake wengi akiwemo Christopher Katongo na Stopila Sunzu ambaye anatarajiwa kujiunga na timu ya Reading ya England.

Saturday, December 22, 2012

Misri yapiga kura ya maoni duru ya pili.


Wananchi wa Misri wanapiga kura tena leo katika duru ya pili ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya iliyoleta utatanishi.
_______________________________________________________________________
Katiba hiyo imepata idhini ya Rais Muhammad Mursi na inaungwa mkono na chama chake cha Muslim Brotherhood, lakini wapinzani wanasema ina makosa.
Watu wa Misri wanapiga kura leo kukubali au kukataa muswada wa katiba ambayo imeigawa nchi.
Upigaji kura unafanyika katika majimbo 17 ambayo hayakupiga kura Jumamosi iliyopita.
Maeneo hayo yanaonekana kuwa hayapendi mabadiliko na yanaunga mkono zaidi chama cha Muslim Brotherhood.
Wafuasi wa Rais Mursi wanasema katiba mpya itarudisha utulivu nchini Misri, lakini upinzani unadai kuwa katiba hiyo haitoi hifadhi kwa wanawake wala uhuru wa kujieleza.
Matokeo yasiyo rasmi ya duru ya kwanza, yanaonesha kuwa wapigaji kura asili-mia-56 wameikubali.
Lakini watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache, na upinzani unalalamika kuwa kulifanywa udanganyifu.

Ofisi ya simu yashambuliwa Nigeria


Shambulio la kujitolea mhanga limefanywa kwenye ofisi ya kampuni ya simu za mkononi katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeriua.
________________________________________________________________________
Polisi wanasema mshambuliaji aliyejitolea mhanga, alisukumiza gari lake wenye ofisi ya kampuni ya Airtel.
Taarifa zinasema kampuni nyengine piya ililengwa.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulio kwa miaka kadha kaskazini mwa Nigeria, limewahi kulenga makampuni ya simu za mkononi likisema kuwa kampuni hizo zinasaidia askari wa usalama kuwakamata wapiganaji

Urusi yataka Sudan Kusini ichunguze



Urusi imetoa wito kwa Sudan Kusini iwape adhabu wale waliohusika na kudungua helikopta ya Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa na kuwauwa Warusi wane waliokuwamo humo.
________________________________________________________________________
Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Urusi ilisema kuwa uchunguzi unafaaa kufanywa sawasawa.
Umoja wa Mataifa ulisema kuwa helikopta hiyo ilidunguliwa na jeshi la Sudan Kusini katika jimbo la Jonglei.
Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Barnaba Marial Benjamin, alisema hapo jana kwamba sababu ya tukio hilo haijulikani na kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikiruka katika eneo lenye wapiganaji. 
chanzo-bbc. 22 Disemba, 2012 - Saa 15:45 GM / tz10:22PM

Thursday, December 20, 2012

BREAKING NEWS: 

Godbless Lema ashinda kesi yake ya rufaa na kurudishiwa Hadhi yake ya Ubunge - Jimbo la Arusha Mjini, Wanachama wa CCM waliomfungulia mashtaka waamriwa kulipa gharama zote za kesi toka ilipoanza.


Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema,
CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia.

FAST jet yawatakia sikukuu njema na mwaka mpya 2013.

FAST jet yavunja rekodi Tanzania kwa kusafirisha abiria kwa bei cheee..

Ama kweli hii ndio FAST jet, karibuni, Hongereni wamiliki / wawekezaji wa hizi ndege.

Sasa hata Mtanzania na mtu wa kipato cha chini kabisa aweza kusafiri kwa njia ya anga kwa kutumia FAST jet.

Wednesday, December 19, 2012

Wadau hapo napo ni kitu cha msimbazi, shekere, mwekundu, shuka la mmasai... nakadhalika...

Haya wadau, mambo si hayo sasa kitu DOLA tuuuu.


                Kibonzo cha leo.

Tuesday, December 18, 2012

WADHANI HAYA MAJANI YAKILETWA DAR KUNA HAJA YA KUTUMIA A/C



KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, Desemba 15-16, 2012, katika Hotel ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, imemaliza kikao chake Desemba 16, usiku. 

Pamoja na kwamba maazimio yote ya kikao hicho yatatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Desemba 18, 2012, huu ni ufafanuzi wa awali kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazowakanganya wanachama na Watanzania kwa ujumla, zilizoandikwa tangu jana Jumapili na Jumatatu, katika baadhi ya vyombo vya habari.

Mbali ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea taarifa ya hatua kadhaa za utekelezaji wa maazimio yatokanayo na vikao viwili vilivyotangulia, Kamati Kuu pia ilijadili hali ya siasa nchini, mchakato wa Katiba Mpya na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya mwenendo wa chama kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambapo ilijadili pia kasoro za utendaji wa viongozi wa chama katika Wilaya ya Karatu.
 

Kamati Kuu ilichukua uamuzi wa kusimamisha uongozi mzima wa Wilaya ya Karatu na kuweka shughuli za utendaji wa chama chini ya uangalizi wa Kamati Kuu mpaka hapo itakapotolewa maagizo mengine baadae.

Aidha, Kamati Kuu pia ilipokea na kujadili mwenendo wa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa taasisi za kiserikali wanaotokana na CHADEMA, hasa katika masuala ya ardhi na maji Wilayani Karatu.

Kikao pia kilibaini kuwa taarifa zinazohusu masuala hayo ya maji na ardhi ni tofauti na namna zilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari. Aidha kutokana na mjadala, iliazimiwa hatua kadhaa zichukuliwe, ambazo umma utaarifiwa katika tamko la Kamati Kuu litakalotolewa kupitia waandishi wa habari.

Imetolewa,Desemba 17, 2012, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
EBU ONGEZA LAKO NA WW KWENYE HII BARUA KABLA HAIJAMFIKIA MUSIKA HUYU .

Dear mwl.nyerere                                  DECEMBER 2012


Tangu uondoke hali hapa tz imebadilika



1:Siku hizi mlima kilimanjaro uko kenya

2:Ziwa nyasa liko malawi

3:Tazanite iko kenya

4:Tanesco ni ya lowassa umeme unakatwa kila sekunde

5:Rais wetu siku hizi anaishi airport

6:Baba nasikitika kukuambia wale wahuni uliowakataa 1995 leo ndio viongozi

7:Nasikia ata kaburi lako halipo tz

8:Siku hizi ikulu wageni waalikwa ni kina Diamond ,wema sepetu ,ray c,hasheem thabit na bi kidude.:

9:Bei ya vitu imekua juu sana wa tanzania wanakufa njaa ,,

10:Mashirika ya Umma yanahujumiwa na wenye uchu


11:Ajira wanapeana kindugu/kwa kujuana

12:Majambazi wamekuwa wengi sana....

13: Wanasema alie nacho huongezewa zaidi

14:....................????........!!!!!



       >>>>>
R.I.P MWL.NYERERE

nawasilisha
@MZALENDO MT
Z



NDEGE YA TANAPA YAANGUKA PORINI , RUBANI ATOKA MZIMA 
Rubani wa ndege ndogo aina ya DASH 5H mali ya TANZANIA NATIONAL PARK (TANAPA) , Athuman Bujwanga (47) mkazi wa mahale kigoma, anusurika kifo baada ya ndege hiyo aliyokuwa akiiendesha kupata hitilafu ikiwa angani na kuanguka kando ya mto Nsemulwa nje ya mji wa Mpanda Mkoani Katavi.




Monday, December 17, 2012

MUONGOZAJI na mtayarishaji wa filamu za Kibongo, Selles Mapunda “Director of Directors” (Pichani) anatafutwa na Polisi baada ya kushutumiwa kumbaka msanii chipukizi "Nancy Njozi" maeneo ya Mwananyamala.


Kwa mujibu wa tovuti ya filamu central, Binti huyo baada ya tukio hilo alikwenda kituo kidogo cha Polisi CCM Mwinyijuma na kupewa RB MWJ/RB/8361/2012 TUHUMA KUBAKA, baadae kesi ikahamishiwa kituo kikubwa cha Polisi Osterbay na kupewa taarifa OB/RB/2012 na OB/IR/11918/2012 KUBAKA.
Picha ilikuwa hivi: Mapunda aliaandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook HELLO! BAADA YA KUKAMILIKA KWA FILAMU YA “THE RETURN OF J-LO” SELLES BUSINESS INC. INAANDAA FILAMU MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA “CROSS OF LOVE” FILAMU ITASHIRIKISHA WASANII NGULI HAPA NCHINI KAMA WEMA SEPETU, DIVA E.T.C PIA KUNA NAFASI ZA WASANII WACHANGA 15.

Sunday, December 16, 2012

   SALAAM:
Chief Executive Officer (CEO) - Ndugu Remmy Tarimo
  KIBO MEDIA GROUP COMPANY LIMITED, na wafanya kazi wa makampuni yote ya "KIBO MEDIA GROUP" wanakutakia X-MAS NJEMA AND HAPPY NEW YEAR 2013. TUNAWAPENDA WOTE WASIKILIZAJI , WATAZAMAJI NA WATUMIAJI BIDHAA ZETU BORA KABISA. 
"Fahari ya Jamii".

Saturday, December 15, 2012

Tukio - 08/12/2012
Bwana harusi Jeremia akiwa amepozi na Boss wake Ndug. Palemo Beda. A.K.A Managing Director at Oxford Driving Collage, Kila la kheri.


Tukio - 08/12/2012
Heee, hapo MD wa Oxford Driving ambaye ni best yangu mkubwa sana hapa Jijini Dar, unajua ananiambiaje, eti Tarimo na wewe jitahidi UOE, hahahaaaa..

Tukio - 08.12.2012
Jeremia akipozi kwenye picha ya pamoja , mkewe na wadau wengine.


Tukio: 08/12/2012
Jeremia  akiwa na mai wafe wake Upendo, waacha weee full raha.

Tukio - 08/12/2012
Jmani hilo ni pozi tu Kijana Jeremia, mkewe na wadau.

Tukio - 08/12/2012
Kaka yake Bibi harusi , anajidai haamini kama dada yake keshachukuliwa na Jeremia, hadi raha.

Tukio - 08/12/2012
Heeee, Kijana wa kisukuma (Mwaveja sana) akimbeba mai wife wake kwenye pozi la picha.

Tukio - 08/12/2012
Heee, wadau Banda na Edwin Kavishe, wanafanya kazi na Bwana harusi ndug. Jeremia.

Tukio - 08/12/2012
Raha sana ndugu Edwini na mdogo wake kwenye harusi ya Jeremia.

Tukio - 08/12/2012
Mdau mimi Remmy nikimsalimia Bwana harusi Jeremia, daah nilitamani ingekuwa ni mimi..

Tukio - 08/12/2012
Bibi harusi, Mrs Jeremia Shija, ndugu Banda, Mdau Remmy na jembe lenyewe JEREMIA ktk pooooooz.