MUONGOZAJI
na mtayarishaji wa filamu za Kibongo, Selles Mapunda “Director of
Directors” (Pichani) anatafutwa na Polisi baada ya kushutumiwa kumbaka
msanii chipukizi "Nancy Njozi" maeneo ya Mwananyamala.
Kwa
mujibu wa tovuti ya filamu central, Binti huyo baada ya tukio hilo
alikwenda kituo kidogo cha Polisi CCM Mwinyijuma na kupewa RB
MWJ/RB/8361/2012 TUHUMA KUBAKA, baadae kesi ikahamishiwa kituo kikubwa
cha Polisi Osterbay na kupewa taarifa OB/RB/2012 na OB/IR/11918/2012
KUBAKA.
Picha
ilikuwa hivi: Mapunda aliaandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa
Facebook HELLO! BAADA YA KUKAMILIKA KWA FILAMU YA “THE RETURN OF J-LO”
SELLES BUSINESS INC. INAANDAA FILAMU MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA “CROSS
OF LOVE” FILAMU ITASHIRIKISHA WASANII NGULI HAPA NCHINI KAMA WEMA
SEPETU, DIVA E.T.C PIA KUNA NAFASI ZA WASANII WACHANGA 15.
No comments:
Post a Comment