Saturday, December 22, 2012

Urusi yataka Sudan Kusini ichunguze



Urusi imetoa wito kwa Sudan Kusini iwape adhabu wale waliohusika na kudungua helikopta ya Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa na kuwauwa Warusi wane waliokuwamo humo.
________________________________________________________________________
Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Urusi ilisema kuwa uchunguzi unafaaa kufanywa sawasawa.
Umoja wa Mataifa ulisema kuwa helikopta hiyo ilidunguliwa na jeshi la Sudan Kusini katika jimbo la Jonglei.
Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Barnaba Marial Benjamin, alisema hapo jana kwamba sababu ya tukio hilo haijulikani na kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikiruka katika eneo lenye wapiganaji. 
chanzo-bbc. 22 Disemba, 2012 - Saa 15:45 GM / tz10:22PM

No comments:

Post a Comment