Ofisi ya simu yashambuliwa Nigeria
Shambulio la kujitolea mhanga limefanywa kwenye ofisi ya kampuni ya simu za mkononi katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeriua.
________________________________________________________________________
Polisi wanasema mshambuliaji aliyejitolea mhanga, alisukumiza gari lake wenye ofisi ya kampuni ya Airtel.
Taarifa zinasema kampuni nyengine piya ililengwa.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulio kwa miaka kadha kaskazini mwa Nigeria, limewahi kulenga makampuni ya simu za mkononi likisema kuwa kampuni hizo zinasaidia askari wa usalama kuwakamata wapiganaji
No comments:
Post a Comment