Misri yapiga kura ya maoni duru ya pili.
Wananchi wa Misri wanapiga kura tena leo katika duru ya pili ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya iliyoleta utatanishi.
_______________________________________________________________________
Katiba hiyo imepata idhini ya Rais Muhammad Mursi na inaungwa mkono na chama chake cha Muslim Brotherhood, lakini wapinzani wanasema ina makosa.
Watu wa Misri wanapiga kura leo kukubali au kukataa muswada wa katiba ambayo imeigawa nchi.
Upigaji kura unafanyika katika majimbo 17 ambayo hayakupiga kura Jumamosi iliyopita.
Maeneo hayo yanaonekana kuwa hayapendi mabadiliko na yanaunga mkono zaidi chama cha Muslim Brotherhood.
Wafuasi wa Rais Mursi wanasema katiba mpya itarudisha utulivu nchini Misri, lakini upinzani unadai kuwa katiba hiyo haitoi hifadhi kwa wanawake wala uhuru wa kujieleza.
Matokeo yasiyo rasmi ya duru ya kwanza, yanaonesha kuwa wapigaji kura asili-mia-56 wameikubali.
Lakini watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache, na upinzani unalalamika kuwa kulifanywa udanganyifu.
No comments:
Post a Comment