Michezo: Tanzania yaifunga Zambia 1-0
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeilaza timu ya taifa ya Zambia,
Chipolopolo kwa bao moja kwa bila katika mechi ya kirafiki ya kimataifa
iliyochezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Katika mechi hiyo bao pekee la washindi, lilipatikana sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza likitiwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa.
Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto,Frank Domayo na Salum Abubakar waliichosha ngome ya Zambia kwa kuelekeza mashambulizi mengi, langoni mwa Chipolopolo.
Mrisho Ngassa kama angekuwa makini zaidi angeweza kuipatia timu yake bao la mapema zaidi.
Timu ya Zambia ilichezesha nyota wake wengi akiwemo Christopher Katongo na Stopila Sunzu ambaye anatarajiwa kujiunga na timu ya Reading ya England.
No comments:
Post a Comment