Wednesday, August 29, 2012




UJUMBE KUTOKA KWA MWESHIMIWA RAIS TAREHE: 27.08.2012

Namnukuu ndugu Rais Jakaya M. Kikwete.

Ndugu Mwananchi, Sensa hii ni kwa watu wa rika zote, jinsia zote na dini zote na kumbuka kila Mwananchi ana haki ya kuhesabiwa. Hakikisha unahesabiwa!

Utani kwenye SENSA...!!


Ubunifu zaidi..!!


Anasikiliza nn sasa...!!


Duuuh, kazi ipoooooo...!!


Unasemaje mdau...............!!!!  na imeishia wapi sasa........!!!


Usingizi huu , nyie endeleeni tu.....sidhani kama tutaamka........

Saturday, August 25, 2012

Sala zenu zinahitajika, samahani lakini. Inasemekena eti Diamond apelekwa Marekani kutibiwa. Ashindwa kufanya show Dar aondoka kwa siri Wema na Jocate wazuiwa kusafiri nae.

Kibonzo chetu..



SASA NATAKA NIONE KAMA TAMKO LA SERIKALI LITAPUUZWA, "NANUKUU" ATAKAYE LETA UVUNJIFU WA AMANI WAKATI WA ZOEZI LA KUHESABU WATU "SENSA-2012" ATAENDA JELA KIFUNGO KISICHOPUNGUA MIAKA MITANO (5).

"Nawanukuu hawa mabwana..."
"Waislamu sisi ndio wengi, lakini wingi wetu ni kama wa Inzi na sio kama ule wa Nyuki na msingi wa matatizo yetu ni kukosekana umoja kati yetu ndio maana tubaburuzwa. Mtaniwia radhi hata Msikiti wa Mtambani niliwaambia wengi wetu ni wanafiki..." Maalim Seif mara baada ya Ibada ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mtoro, Kariakoo Dar es Salaam



Duuuh, nakumbuka mbaaaaaali sana...!, sijui wewe msomi mwenzangu.



OMBAOMBA MAARUFU MZEE MATONYA,
AFARIKI DUNIA.......



Friday, August 24, 2012

Thursday, August 23, 2012


DUUUUH...!! HII GARI INA MIAKA 14, HII TAIRI HAIJAWAHI PATA PANCHA..


OUR UP-COMING PASTER...!!
IN THE NAME OF JESUS "PEPO OUT...!



Wednesday, August 22, 2012

Mpango mzima huoooooooooooooo...!


Wdau husema  PESA ni mzizi wa kila kitu, noooop YESU ndie kila kitu kwa aaminiaye..!! to be honest.

Monday, August 20, 2012

Wednesday, August 15, 2012











  
MISRI HUYU NDIYE NYOKA HATARI NA MKUBWA SANA DUNIANI KOTE (ANACCONDA) ALIELETA MADHARA MAKUBWA SANA
 

==============================================
Kama utakumbuka ndani ya mwaka huu 2012 Nyoka aina ya Anacconda, anayeishi ndani ya maji baharini, alileta madhara makubwa sana ikiwa ni pamoja na kuvizia na kumeza watu zaidi ya 530 wengi wakiwa ni wageni waliokuwa wakipunga upepo ufukweni mwa bahari na madereva zaidi ya 125 mwaka huu huu wa 2012, kwa bahati nzuri ilipofika tarehe 12/8/2012 nyoka huyu tishio aliweza kuuawa na wanajeshi na raisa wa Misri, baadae aliwekwa kwenye gari kubwa sana la kijeshi na (kama anavyonekana) na kutembezwa sehemu mbali mbali za nchi hiyo, na baadae alipelekwa kwenye makumbusho ya Taifa hilo.
=========================================================================

HII NI CHOPA YA CHADEMA MAMBO YA M4C
GODBLESS LEMA: Akikagua chopa ya chadema waliyonunua London kwajili ya M4C.


NI MOJA YA NCHI ZA AFRICA MASHARIKI TUUUU..!! A/C SIO BUNGENI TUU JAMAN TWALIPA KODI MJUE.
Hiki ni kituo cha kusubiria basi kwenye moja ya nchi zilizoendelea, Ukiwa unasubiri basi humo ndani unapigwa na A/C ya kutosha... Je hii itafika lini kwetu??


....WATANZANIA MPO TAYARIIIIIIIII...


SINEMA KATI YA DR. ULIMBOKA A.K.A STALING NA AFANDE KOVA  ITAANZA SOON..!!

................Stay watching party two is coming soon.................

.....This August 2012....

Tuesday, August 14, 2012


KIBAHA READ FOR OLYMPIC IN LONDON


















TANZANIA TUNA WATU WENYE VIPAJI BASI TU KAMA HUYU ANGEENDA LONDON KWENYE OLYMPIC ASINGERUDI NA MEDALI KWELI?
 MGANGA WA JADI  AJISEVIA BILA HATA YA KUTONGOZA
kale katabia ka wadada kwenda kwa waganga kutafuta mume nk..... habari yao hiyo hapo.

Wadau, ukweli hakuna jipya chini ya jua.



KIFARU MAAJABU YA MWENYEZI MUNGU.

Nyinyi mafisadi huyu kifaru wa aina yake yuko mbuga yaaaaaaa... niwaambie ili mukamwibe mumuuze ulaya, weee nimewashtukia.

  .    Kitu Olympic         


Monday, August 13, 2012

MZUNGU NAJIFUNZA KUPIKA UGALI HAPA MOSHI.

Hahahaaaa alijitahidi saana, cha kuchekesha maji yalivyochemka aliepua na kuweka unga na kusongaaaaaa, kisha akarudishia jikoni, holaaaaaaaaa madonge dongeeeeee..

Sunday, August 12, 2012


Ki ukweli nakiri “MWIHIMBILI HOSPITAL” bado kuna MGOMO baridi, amini usiamini, nilikuwa hopo Ijumaa tarehe 10/08/2012 saa 7:27Hrs, rafiki yangu alipata ajali na kuvunjika mkonowake wa kulia, toka saa 7:27Hrs tuliondoka Muhimbili saa 14:13Hrs, ama kweli niligundua Muhimbili “MGOMO” MGOMO…. Upo. Mwihimbili wale mnaokwenda naomba museme ukweli, watu wanateseka jaman, hadi naandika habari hii niliumia sana, watu wanalala chini hadi mlangoni bila huduma jaman, MASIKINI hao na ndio walipa kodi….., matajiri mnatibiwa nje ya nchi.
La ajabu mgonjwa aliepata ajali anapoletwa MOI cha ajabu Daktari hana hata Gloves, jamani tunakwenda wapi, nilishuhusia muuguzi mwenye huruma akimmwagia mtu anaevuja damu spirit na kumfuta LIVE mikono mitupu na pamba bila Gloves, nilitamani kulia, Tanzania / viongozi naombeni jibu, hapo nilikuwa hospitali ya Taifa Muhimbili tu, je za mikoani!!!!?? chonde chonde jamani.

ASANTENI KWA KUNIELEWA....
********            ********    **********     *************     ***********        **********



  AREJEA Dk. Steven Ulimboka, aapa kuendelea na harakati zake


Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa amebeba maua, nakuzungukwa na madaktari wenzake na wananchi wa kawaida, alipowasili leo Jumapili Agosti 12, 2012 , kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini. Alisema yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.
NAPE AJICHANGANYA..!!


“Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za "kisanii" kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo palifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

Wednesday, August 8, 2012

DUUU.. MSHUWA AKATAA DIAMOND KUTUMIA JINA LAKE.


SOO juu ya soo! Baada ya mkali wa Bongo Fleva, Nasibu ‘Diamond’ Abdu 
kumchana baba yake, Abdu Juma katika gazeti dada na hili Ijumaa, mzazi huyo ameibuka na kumtaka mwanaye asitumie jina lake tena, Risasi Mchanganyiko linashuka kwa kujiamini.
Akizungumza kwa uchungu hivi karibuni, nyumbani kwake Magomeni, Dar, mzee Abdu alisema kitendo cha Diamond kumkana kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa yeye siyo baba yake kilimuudhi sana na haoni sababu ya kuendelea kutumia jina lake.
SAUTI YA MZEE ABDU KUTOKA MAGOMENI
“Nasibu (Diamond) ni mwanangu na hilo jina nimempa mimi, nimemlea mwenyewe na kumpeleka shule, lakini leo ananikana. Kama ndivyo, aache kutumia jina langu.
“Nilimtumia meseji baada ya kuona gazeti hilo mtaani nikamwambia atafute jina lingine maana ameshasema hanitambui kama baba yake. Namshangaa sana huyu mtoto, hata sitaki kumsikia lakini ipo siku nitamtafuta nimweleze kwa mdomo.

“Sina shida na umaarufu wake kama anavyodhani, yeye aendelee na mambo yake, kwanza hana faida na mimi, si amedai aliyemlea ni mama yake? Basi aendelee naye sitaki kupigizana naye kelele,” alisema mzee Abdu.

KUMBE DIAMOND ALIWAHI KUMPELEKA WEMA KWA MZEE ABDU!
Katika kuthibitisha kwamba, Diamond anatambua yeye ni baba yake, mzee Abdu alisema, alipomvalisha Wema Sepetu pete ya uchumba alimpeleka nyumbani kwake kumtambulisha.
“Diamond alikuja kunitambulisha Wema kuwa ndiye mchumba wake ikiwa ni baada ya kumvisha pete na tulipiga naye picha,” alisema.
Hata hivyo, alikataa kutoa picha hizo kwa waandishi wetu ili zitumike gazetini.
Aliongeza: “Mama yake huwa tunaongea vizuri tu, hata siku hiyo (aliyomwandikia meseji Diamond) nilimpigia mzazi mwenzangu na kumweleza, akaniambia niachane na mambo ya magazeti na redio, mimi nitabaki kuwa baba yake.
“Jambo hilo sikubaliani nalo hata kidogo, kwa sababu tayari amenidhalilisha, hata mtaani kwangu watu wanajua kuwa mimi ni baba yake na bado wanaendelea kuniita Baba Diamond... naitika kwa shingo upande tu,” alisema Abdu.

AMWACHIA MUNGU
“Diamond amefanya kitu kibaya na anatakiwa kujua kuwa nimeumizwa sana na kitendo chake, lakini sina namna. Mimi namwachia Mungu, yeye ndiye anayejua kuwa ni mwanangu au lah.
“Mzazi yeyote lazima ataumizwa na maneno mabaya ya mwanaye kama alivyofanya yeye. Si maungwana watu wengine kuiga tabia ya namna hii. Diamond amenidhalilisha,” alisema
.

AJALI MBAYA BASI LABEBA WATU ZAIDI YA 100, 17 WAFA NA 78 WAJERUHIWA.



Ajali ya basi la sabena lapoteza maisha ya watu 17, na 78 wajeruhiwa

Watu 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM kupata ajali na kupinduka. 

Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.

Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.


   DOGO UNAAMUAJE WEWE SASA JAMAN...!!


POLISI TUNAOKOA MADHARA YASITOKEE             . 














Jamaa alifumaniwa pande fulani jijini dar, duuh hii ni aibu sana jaman, polisi ilibidi waingilie kati, mwenye mke alitaka kutoa maamuzi ndivyo sivyo.. kula baaaata..!!! hahahaaaa.
BILA MAKUU.


Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa kijijini na wanakijiji wenzake, ama kweli jamaa hana makuu, safi sana.

MBEYA
BOMBA FM HONGERENI. WASHIKA NAFASI YA PILI MAONYESHO YA NANE NANE.






































Wadau wa BOMBA FM "Washukuru kwa ushirikiano wenu, wasema hii zawadi  ni kwa wadau wote wa BOMBA FM RADIO 104.0 Mhz MBEYA"

JINYEE  SASA TUKIKATAZA PIKIPIKI HII KUINGIA NCHINI ITAKUWAJE
















Ona majina mengine bwannaa ni ya ajabu sanaaaa...!, "made from china."TBS mpoooo..!! hiyo iko hapa hapaaa...

HATARI LAKINI NI MCHEZO TOSHA....


















Mchezo tosha... Huyu dogo huwa anakula hadi nauli.. Na huu ndo mchezo tosha daily kudandia mabasi...

MADHARA YA KUHAMAHAMA VYAMA VYA SIASA.....
















JAMAA ALIKUWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA AKASAHAU AKASEMA, "NAMNUKUU".. CCM OYEEEE........, WATU AHAAAAAAAAAAAAAAAA........!!

KIBONZO CHETU.















Sawa baba, najitahidi ..!!



MOROGORO ASKARI POLISI AJINYONGA






Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga
Danstan Shekidele
Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika.

Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.

Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.

Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.

Alisema baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.

Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.

“Pamoja na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema Kamanda Shilogile.

Alipoulizwa kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.

Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Tuhuma nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.

Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.

Tuhuma nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku.

**********                                    ****************                      *******************

MGOGORO MALAWI NA TANZANIA.


















UNA MAONI GANI JUU YA HALI YA SINTOFAHAMU KUHUSU MGOGORO UNAOENDELEA KATI YA MALAWI NA TANZANIA.



MBOZI  WATU WAWILI WAJERUHIWA NA SIMBA.

Watu wawili waishio Kijiji cha Shasya,Kata ya Halungu,Wilaya ya Mbozi Mkoania Mbeya wamenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya na mnyama anayedhaniwa kuwa simba kijijini hapo.

Akizungumzia tukio hilo Diwani wa Kata ya Halungu mheshimiwa Samson Simkoko,amewataja waliojeruhiwa ambao wamefahamika kwa jina moja ni pamoja na Nzowa na Simkoko,tukio lililotokea katika msitu wa Shasya wakiwa katika shunguli ya kuwinda Nguruwe Pori mnamo Agosti 6 mwaka huu.

Katika sakata hilo Simba huyo alianza kuwashambulia na katika mapambano hayo watu hao wamejeruhiwa vibaya,licha ya kujikongoja hadi kijijini na kuomba msaada na kukimbizwa katika Hospitali ya Mbozi Mission,ambapo hali zao zimetajwa kuendelea vema.

Aidha Diwani Simkoko alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Halungu,na majeruhi kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na kisha alitoa taarifa katika Ofisi ya Maliasili,Wilaya ya Mbozi na sasa wanafanya msako mkali kwa kushirikiana na wananchi kumsana Simba huyo.

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.

RUNGWE  MTOTO AHOFIWA KUFA MAJI.

Mtoto anayefahamika kwa jina la Allan Mwakalasya(17),mkazi wa Kijiji cha Mpandapanda,Kata ya Kiwira,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amehofiwa kufa maji baada ya kwenda kuogelea katika maporomoko ya Mto Kiwira.

Tukio hilo limetokea Julai 6 mwaka huu majira ya saa 6 mchana, marehemu akiwa na mwenzake walienda kuogelea katika maporomoko ya mto huo,ndipo alipopiga mbizi mara tatu na mara nne aliingia akiwa ametanguliza kichwa alichukua dakika tano kuibuka na kunyosha mikono juu na kuzama moja kwa moja na mpaka sasa hajapatikana.

Baada ya tukio hilo watoto wenzake walichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mama yake mzazi Bi. Emma Kosiyo(43) na mjomba wake Bwana Albert Mwakajila(60),ambao walienda eneo la tukio na kumtafuta Allan bila mafanikio na kuamua kutoa taarifa katika Ofisi ya kijiji ambapo ilipigwa Mbiu na wananchi kukusanyika eneo hilo la tukio huku wataalamu wa uzamiaji majini wakimtafuta bila mafanikio.

Takribani siku wananchi wameendelea na zoezi hilo na wakati huo wanatarajia kuonana na Viongozi wa kimila ili kusaidia kuendelea kuutafuta mwili wa Allan.

Hata hivyo taarifa hizo zimetolewa katika Kituo cha Polisi cha Kiwira, na Askari wa kituo hicho wameendelea kushirikiana na wananchi kuutafuta mwili huo.

Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe Mbeya.

DODOMA.
DKT. BILAL AFUNGA RASMI MAONYESHO YA SHEREHE ZA WAKULIMA JIJINI DODOMA MAARUFU KAMA"NANE NANE"


Makamu wa Rais, Mh. Dkt Garib Bilal  afunga rasmi maonyesho ya sikukuu ya wakulima mjini dodoma leo tarehe 8/8/2012.