Wednesday, August 8, 2012


AJALI MBAYA BASI LABEBA WATU ZAIDI YA 100, 17 WAFA NA 78 WAJERUHIWA.



Ajali ya basi la sabena lapoteza maisha ya watu 17, na 78 wajeruhiwa

Watu 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM kupata ajali na kupinduka. 

Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.

Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.

No comments:

Post a Comment