RUNGWE MTOTO AHOFIWA KUFA MAJI.
Mtoto
anayefahamika kwa jina la Allan Mwakalasya(17),mkazi wa Kijiji cha
Mpandapanda,Kata ya Kiwira,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amehofiwa kufa
maji baada ya kwenda kuogelea katika maporomoko ya Mto Kiwira.
Tukio
hilo limetokea Julai 6 mwaka huu majira ya saa 6 mchana, marehemu akiwa
na mwenzake walienda kuogelea katika maporomoko ya mto huo,ndipo
alipopiga mbizi mara tatu na mara nne aliingia akiwa ametanguliza kichwa
alichukua dakika tano kuibuka na kunyosha mikono juu na kuzama moja kwa
moja na mpaka sasa hajapatikana.
Baada
ya tukio hilo watoto wenzake walichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa
kwa mama yake mzazi Bi. Emma Kosiyo(43) na mjomba wake Bwana Albert
Mwakajila(60),ambao walienda eneo la tukio na kumtafuta Allan bila
mafanikio na kuamua kutoa taarifa katika Ofisi ya kijiji ambapo ilipigwa
Mbiu na wananchi kukusanyika eneo hilo la tukio huku wataalamu wa
uzamiaji majini wakimtafuta bila mafanikio.
Takribani
siku wananchi wameendelea na zoezi hilo na wakati huo wanatarajia
kuonana na Viongozi wa kimila ili kusaidia kuendelea kuutafuta mwili wa
Allan.
Hata
hivyo taarifa hizo zimetolewa katika Kituo cha Polisi cha Kiwira, na
Askari wa kituo hicho wameendelea kushirikiana na wananchi kuutafuta
mwili huo.
Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe Mbeya.
No comments:
Post a Comment