MBOZI WATU WAWILI WAJERUHIWA NA SIMBA.
Watu
wawili waishio Kijiji cha Shasya,Kata ya Halungu,Wilaya ya Mbozi
Mkoania Mbeya wamenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya na mnyama
anayedhaniwa kuwa simba kijijini hapo.
Akizungumzia
tukio hilo Diwani wa Kata ya Halungu mheshimiwa Samson
Simkoko,amewataja waliojeruhiwa ambao wamefahamika kwa jina moja ni
pamoja na Nzowa na Simkoko,tukio lililotokea katika msitu wa Shasya
wakiwa katika shunguli ya kuwinda Nguruwe Pori mnamo Agosti 6 mwaka huu.
Katika
sakata hilo Simba huyo alianza kuwashambulia na katika mapambano hayo
watu hao wamejeruhiwa vibaya,licha ya kujikongoja hadi kijijini na
kuomba msaada na kukimbizwa katika Hospitali ya Mbozi Mission,ambapo
hali zao zimetajwa kuendelea vema.
Aidha
Diwani Simkoko alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Halungu,na
majeruhi kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na kisha alitoa taarifa katika
Ofisi ya Maliasili,Wilaya ya Mbozi na sasa wanafanya msako mkali kwa
kushirikiana na wananchi kumsana Simba huyo.
No comments:
Post a Comment