Tuesday, July 31, 2012

WAZEE WA FEVA MMEONAAAAA..!!
SASA MMEMUONA HUYU .. AMAAA.....



Boda boda akiwa na abiria huku kavaa Kisadolini cha lita nne, sijaelewa alikuwa anamaanisha nini ama ni uchokozi tu kwa askari wa usalama barabarani.

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar, Kaskazini Pemba, wakiwa katika chakula cha futari walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar Alihaj Dkt Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ikulu wete Pemba.



DKT. SHEIN AFUTURISHA KISIWANI PEMBA



Rais wa Zanzibar Alhaji Dkt. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kushoto) akijumuika na viongozi na wanachama wa mkoa wa kaskazini Pemba katika chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya wete Pemba jana.


Kwa hisani ya michuzi.


TUNDUMA - MBEYA.MGOMO WA WALIMU,IMEKUWA FURSA KWA VIBAKA KUNUFAIKA. 


Kufuatia Mgomo wa walimu ulioanza jana, wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Mji mdogo wa Tunduma,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya waliamua kuandamana ili kudai haki ya kufundishwa katika maandamano ambayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya mji huo na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.

Hatua hiyo ilijitokeza mapema saa 2 asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri wa Tunduma,walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani ambapo baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi cha mjini hapa kabla ya kufika ofisi za halmadhauri ya mji.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, awali wanafunzi hao walikwenda nyumbani kwa Diwani wa kata ya Tunduma mheshimiwa Frank Mwakajoka (CHADEMA) na baada ya kufanya mazungumzo na mke wa diwani huyo ambaye inadaiwa hakuwepo waliandamana hadi kituo cha polisi na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya mji ambapo msafara huo uliingiliwa na baadhi ya watu walioendesha uporaji huo.
 

Mmoja wa shuhuda hao ambaye alijitambulisha kuwa ni Julius Edward, alidai kuwa baada ya wanafunzi hao kufika katika ofisi  za polisi walipokelewa na kufanya mazungumzo ambayo  maamuzi yake hayakuafikiwa na wanafunzi hao.
 

Alisema baada ya kutoafiki majibu yaliyotolewa na Polisi 
wanafunzi hao waelekea kwenye mzunguko wa barabara uliopo karibu na eneo la ofisi za Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika mpaka wa Tanzania na Zambia ambako walizuia barabara ili magari yasipite.

Usumbufu huo ulidaiwa kujitokeza kwa muda wa nusu saa, hatua ambayo ilisababisha polisi wa kituo hicho kufika eneo hilo na kulazimika 
kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia mabomu mawili ya machozi hali ambayo ilisababisha vibaka kujiingiza na kuaanza uporaji kwa kukimbilia ziliko ofisi za halmashauri ya mji.

Watu hao ambao wameonekana wakivamia ofisi hizo na kuchoma moto baadhi ya mali za halmashauri hiyo huku wakipora  kompyuta 5 za ofisi, pikipiki yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali sambamba na kuvunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya kubebea taka aina FAW  SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo  na gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.
 

Kulingana na tukio hilo vibaka wameweza kuonekana wakipora mali katika ofisi hizo huku wengine wakivunja chumba cha kuhifadhia mizigo mbalimbali na kufanikiwa kuiba mabati na viti na mali nyingi zilizokuwa zikibebwa,huku baadhi yao walionekana wamebeba madumu ya mafuta ya petroli wakitishia kuchoma jengo hilo.
 

Wanacnhi wa mjini hapa wanakumbuka matukio mbalimbali yanayojitokeza katika mji huu kuwa huwa yana leta adhari, kama ilivyo tokea katika matukio machache ya Februari 18, 2005 kufuatia wamachinga watano waliokamatwa Nakonde Zambia na mnao Septemba mosi hadi 3 mtu mmoja aliyefia  katika mahabusu ya Nakonde nchini Zambia.
 

Mji wa Tunduma umekuwa kinala cha  matukio ya vurugu  na uvunjifu wa amani linapotokea jambo lolote hali ambayo huchangiwa na
   watu wanaojiita wana harakati kuongoza vikundi vya watu ambao huaribu na kupora mali za watu.

Mkurugenzi wa mji huu Aidan Mwanshiga alipotakiwa kuelezea uharibifu hu alisema kuwa 
  tadhimini ya uharibifu uliotokea inafanywa na taarifa rasmi itatolewa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akizungumzia tukio hilo alisema kuwa tukio hilo haliwezi kuvumiliwa kutokana na kuwa maandamano ya wanafunzi hayawezi kupelekea kuvunjwa kwa ofisi za serikali bali kuna watu ambao wametumia mwanya huo ili kupora mali.

Aidha Kamanda Diwani alisema mbali ya uharibifu wa mali za Mamlika ya mji wa Tunduma hakuna madhala mengine yaliyotokea ikiwa ni pamoja na majeruhi au vifo vilivyojitokeza.


Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Momba Bwana Abiud Saideya amesema amesikitishwa sana na kitendo cha uharibifu wa nyaraka na mali za serikali na kudai kuwa hizo ni mali za wananchi,hivyo atahakikisha wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka amesema leo kutakuwa na mkutano wa hadhara wa kuzungumzia vitendo vilivyofanywa na watu hao ambao wamesababisha hasara kubwa kwa halmashauri.  

Wakati huo huo katika Kata ya Vwawa wanafunzi wa shule za Ichenjezya na Haloli waliandamana hadi ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mbozi na baada ya maandamano hayo walirejea shuleni kwao kwa amani huku wakisindikizwa na Polisi.

Wanafunzi hao walidai kuwa walimu wao walifika shuleni lakini hawakuwa tayari kufundisha wakiwaambia kuwa hawatafundisha kwa vile wapo kwenye mgomo hivyo waliwashauri waandamane hadi ofisi za halmashauri kudai haki yao hiyo.

Vilevile habari kutoaka Jijini Mbeya zimeeleza Mbeya zimeeleza kuwa mgomo ulianza mapema jana asubuhi, ambapo walimu walifika shuleni na kusaini kitabu cha mahudhurio kisha kukaa kimya huku wakiawaacha wanafunzi wakilandalanda bila cha kufanya.

Na: Ezekiel Kamanga,Tunduma

GAZETI LA DIRA:
KASHFA YA KUHONGWA WABUNGE LAWATAJA - Zitto , Ole sendeka , Sarah Msafiri na Anne Kilango




Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto Kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii tu.

Kwa upande mwingine limeeleza kuwa Katibu mkuu wa Chadema Dk. Slaa amesema ikiwa itabainika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.
Kwa hisani ya G Sengo .



MALAYSIA: HAWA NDIO MAPACHA WALIOTENGANISHWA.



 Waziri wa Afya wa Malaysia Liow Tiong Lai akiwa hospitalini kuwaona watoto hao baada ya kufanikiwa kutenganishwa.
Mara kadhaa watoto mapacha wanapozaliwa wakiwa wameungana huwa inakua kazi nzito kuwatenganisha na wakati mwingine huwa wanafariki wakiwa kwenye zoezi la kutenganishwa na wengine wanapoteza maisha kutokana na pesa ya hayo matibabu ya gharama kukosekana lakini kwa Malaysia wamepata bahati wakati huu.

Kuna watoto walizaliwa April 2011 wakiwa mapacha walioungana mguuni ambapo baada ya juhudi za Madaktari mabingwa kufanya upasuaji, wamefanikiwa kuwatenganisha hawa malaika Muaiman na Muaimin na wakabaki kuwa hai.

Idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wazazi waliokua wanaifatilia habari ya watoto hawa wamejawa na furaha baada ya kusikia hilo zoezi limefanikiwa.

Pamoja na kwamba upasuaji umefanikiwa, ugumu ulikuwepo kwenye sehemu ya kuhifadhia mkojo mwilini ambayo pia ilikua imeungana toka wamezaliwa, sasa hivi wapo chini ya uangalizi wa kitaalam mpaka hali yao itakapo ruhusu kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa mujibu wa Star news paper.
__________________________________________________________ 

Kwa hisani ya Millard.








Mdau Richard Mpungu, aamua kuuaga ukapela, walipendeza sana yeye na mke wake, kushoto ni mshenga wake Ndugu Amos Millinga.

Monday, July 30, 2012



Mr. Bean (daaah ni  bonge la msanii,






Prof. Lipumba "CUF".




NASHUKURU KWAMBA HAKUNA MBUNGE HATA MMOJA TOKA CUF ANAYE HUSIKA NA KASHFA ZA RUSHWA BUNGENI, LAKINI HATA KAMA AKIWEPO NA IKATHIBITIKA NAAPA TUTAMFUKUZA UANACHAMA.

NASHANGAA VYAMA VILIVYO TAJWA WABUNGE WAKE KUHUSIKA NA RUSHWA BUNGENI WANASUBIRI NINI KUCHUKUA HATUA, SISI KAMA CUF TUNALAANI VIKALI NA TUNATAKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE KWA WOTE WALIO HUSIKA.

Chama cha wananchi cuf kimesema
 kinashukuru kuwa hakuna hata mbunge mmoja kwa tiketi ya chama hicho anaye anahusika na kashfa ya kupokea rushwa bungeni, Ikumbukwe baadhi ya wabunge toka CCM, CDM-CHADEMA NA NCCR MAGEUZI ni miongoni mwa wabunge wanao tuhumiwa katika sakata zito la usaliti kwa wapiga kura wao pale wanapo pokea rushwa ili kupitisha mambo mbali mbali katika kamati wanazo ziongoza.

HEKO CUF KWA KUWA NA WABUNGE WANAOJALI MASLAHI YA WAPIGA
KURA WENU NA TAIFA KWA UJUMLA
ZAIDI KUTUNZA HESHIMA YA CHAMA CHENU CUF.


Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..!!







John Ngahyoma (was a BBC presenter)


Losing our beloved one was our one step back. After reflection we realize that now it is time to take even greater steps forward. It is our duty to honor the man he was by continuing to share what he has taught us. No more tears, only living the life he taught us so well to live. Remembering this one step back will forever keeping us moving many more steps forward. Thank you, we will remember u always. Rest in Peace John Ngahyoma we will love u forever.




SOMALIA.


These people die of hunger...
These people die of starvation of food... 
If u have heart, u will surely share so that at least people would know there are poor people like this suffering without food. Amen!!

Mwanangu eheeee, majua wapo wengi, mshumaa utapika chakula kweli.


Utasubiri saaaana mwanangu.

Daaaah.... Africa mpooo.



Mwanamama mwenye nywele ndefu kuliko wote duniani huyu hapa, je wadada wa kiafrika mnaweza kutunza nywele kama hivi.

               Charles na Mtarajiwa wake Neema Mlay kwenye pozi.




Mdau hongera saana , huyo ni dada yangu wa kule Marangu, anahitaji matunzo na malezi bora, mbarikiwe nyote.


Charles Haule (TBC) amvisha Neema Mlay Pete ya Uchumba


Mpiganaji Charles Haule wa TBC akimvisha Neema Mlay Pete ya Uchumba, inapendeza sana Brother, one love.

Askofu Mkuu Fransisco Padilla - Balozi wa PAPA Tanzania.



Kwa mara ya kwanza Balozi wa papa nchini Tanzania akiwahutubia watoto wapatao 72 waliopata sakramenti ya kipaimara katika kanisa la Petro Oysterbay jijini Dar es salaam.

    Mexico City.                                                                                                     


Je afrika tunatumia maksai kulima, wenzetu wana kuku wakubwa sana wenye uwezo zaidi ya maksai wa Afrika, walijua hilo... najua unataka kujua..ila nakujuza zaidi.

Sunday, July 29, 2012



WE LOVE AFRICA..!!!


Kibonzo cha leo.



Hapo ni CHINA.




Hawa raia wa China wananifurahisha saana, Mbwa nchi nyingine tuna watumia kama walinzi, uchina ni kitoweo kama bucha la nyama za ng'ombe Tz, karibu tule mwayaa..!!



Mchagga weeeeee..!!


Duuh, anapata Lunch na Kambege pembeni, aika mae, puliza puliza kwanza...
DODOMA                                                                                          






Mh. Mizengo Pinda- Waziri Mkuu, akagua ujenzi wa barabara Dodoma, ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.
Baadhi ya sehemu ya daraja la barabara ya dodoma likijengwa.




Mafundi wakiendelea kujenga Daraja la kisasa, manispaa ya Dodoma,  ambako Waziri Mkuu alitembelea ujenzi huo.

(Picha na ofisi ya waziri mkuu).






GODBLESS LEMA  afunguka.....!!




KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK GODBLESS LEMA WA CHADEMA AMEANDIKA HIVI............!! 
NINAMNUKUU.................!!

Naomba hili liwe wazi kwa Watanzania, Ridhiwan Jakaya Kikwete, chini ya kampuni ambayo wanaharakati tutaleta ushahidi wake kwa wananchi wanaotaka ukombozi, wiki hii alikuwepo Jijini Arusha na tayari ana mkataba wa umiliki wa zaidi ya hisa asilimia 45 za kampuni ya Tanzanite One. Hii ni biashara ya Rais wa nchi. Ametumia madaraka yake kwa siri kupisha umiliki huu kupitia mtoto wake. Linaweza kukanushwa na kupingwa lakini muda unafika ambapo umma wa Watanzania utaamua. Hata wakishinda kesi za mahakamani, hawataushinda uamuzi wa umma. CCM inakufa, iko hatua za mwisho kabisa.

Saturday, July 28, 2012


     JE INAWEZEKANA HAWA SIMBA WAKAWA NDIO WATALII AU...!!

 


   JIJINI DAR.


His excellent Paul Kagame, the president of Rwanda, hivi ndivyo Tanzanaia Jijini Dar es salaam - uwanja wa Taifa ulivyofurika, maelfu kwa maelfu ya mashabiki wakiishangilia Yanga kwa kuibuka mshindi wa kombe lako la KAGAME CUP 2012.

















JIJINI DAR LEO 28/7/2012.




Kabumbu lasakatwa kati ya wana Azam watoto wa Bharesa na watoto wa Manji, mtanange huu uliilazimisha Yanga kuongoza kwa bao 1-0 thidi ya Azam FC, na kuifanya Yanga kuibuka mshindi wa Kombe a Kagame 2012, Mshindi atazawadiwa zaidi ya US$ 30,000.

KIKOSI CHA AZAM FC (waendelea kulamba Ice creem)





KIKOSI CHA YANGA...!! MTANANGE ULIKUWA SI WA KITOTO..

Friday, July 27, 2012



THIS IS REAL BAD...!!!


SHE'S STILL INSISTING THAT, SHE LOVES HER BOYFRIEND AFTER DAMAGING

HER FACE.

IS THIS LOVE??????


WOMEN, WOMEN, WOMEN WAKE UP..!






SASAAAAAAAAA..!!


Je ingekuwa ni wewe umekutana na haya ungefanya nini!!!!.
"The Man of God", A.K.A Emmanuel, aendelea kutoa uponyaji wa kiimani kwa maelfu ya watu ulimwenguni kote, mtumishi huyo anaishi Nigeria - Lagos.
Mmmmmh..!!!





Hapa ni kazi tuuu, hakuna mazungumzo.



KIBONZO  CHETU....!! Chezeyeeeya wewe.





HAHAHAAAAA...!! WACHAGGA MPOOOOO....!!




Hapa kwa kweli ni uchaggani, usione body imechoka injini ni mpa babangu.





Mwanaume ajifungua, madaktari washangaa:
Duniani kuna mambo sana, mwanaume huyu amefanyiwa operation na kutolewa mtoto mwenye afya tele.
HATIMAYE RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, AZINDUA KARAKANA YA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION AIR DAR.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Precisio Air baada ya uzinduzi wa karakana yake ndogo Dar, Kulia ni waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe.

CEO wa Global Publisher, Erick Shigongo wa pili kushoto, akizungumza na waandishi wa habari (hawaonekani pichani) juu ya mashtaka ya msanii wa Uganda Jose Chameleon


Hivi ndivyo msanii wa Uganda Jose Chameleon na umati wa watu wengi walivyokwenda Ubalozi wa Tanzania Uganda, hii ilikuwa ni kudai Passport yake iliyoshikiliwa na Promoter wa wasanii Tanzania CEO-Erick Shigongo.

Ila nadhani hii sio sahihi kwenda kudai passport kwa nguvu ktk ubalozi huo, huu ni ukosefu tuu wa nidhamu kwa msanii Jose, biashara zako binafsi usiingize ubalozi na Tanzania kwenye matatizo, wahusika kueni makini.


Kwa kweli Tafakari....!!!!!!!!!!!!!



HAKIMU ATOKA NJE YA MAHAKAMA NA
 KUZICHAPA KAVU KAVU NA 
MWANANCHI.

Habari na Ezekiel Kamanga,Iyula Mbozi.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo,Kata ya Iyula,Tarafa ya Iyula,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Mheshimiwa Grace Kivelege aliuacha Ukumbi wa mahakama hyo na kutoka nje kisha kuanza kuzozana na mwananchi mmoja Bwana Sebastian Kilindu aliyekuwa amefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi.

Sababu ya ugomvi huoni pale Hakimu huyo alipomtaka mshitakiwa Bwana Laurence Julias,kuingia mahabusu ndipo Bwana Kilindu alipinga hali iliyompelekea hakimu kumkunja shingoni na kuamuliwa na mwandishi wa habari hizi,huku wananchi wakishangilia zogo hilo wakitaka Hakimu apigwe kutokana na kinachodaiwa kuwa kajijengea mazingira ya rushwa.

Baada ya kuamuliwa hakimu huyo alimfuata tena Bwana Kilindu na kumkunja mbele ya Kituo cha Polisi cha Iyula,Wilayani Mbozi huku akiporomosha matusi ya nguoni na kushangaza wananchi baada ya kuzivunja sheria ili hali kapewa dhamana ya kuzisimamia.

Aidha,kesi hiyo iliyokuwa ikimhusisha Bwana Laurence ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na baadae kukata rufaa katika Mahakama ya wilaya ya Mbozi na kuachiwa huru lakini alibambikiziwa kesi nyingine akidaiwa kuwapiga wananchi watatu wanaoishia katika Kijiji cha Ichesa wilayani humo.

Mtuhumiwa Laurence amekuwepo jela kwa muda wa mwezi mmoja,ambapo ndugu na jamaa walifika siku ya Jumatatu Julai 23 mwaka huu kwa ajili ya kuomba kumwekea dhamana ambapo Hakimu huyo Bi.Kivelege alikataa na kuwataka wafike siku inayofuata Julai 24 wakiwa na barua ya udhamini.

Aidha,walipofika siku hiyo Julai 24 mwaka huu wakiwa na barua ya udhamini,bado hakuwasikiliza hadi ilipofika majira ya saa 9:30 alasiri ndipo alipotoa hati ya kumtoa gerezani na mshitakiwa kufikishwa Kituo cha Polisi cha Iyula majira ya saa 12:30 jioni na kudhaminiwa na kaka yake mbele ya Mkuu wa kituo hicho Mkaguzi msaidizi Inspekta Uziweli Mwanga ambapo alitakiwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili.

Julai 25 mwaka huu mshitakiwa alifika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili lakini kabla ya kesi Bwana Laurence Julias aliwasilisha barua yenye sababu ya kumpinga hakimu huyo,ambapo sababu ya kwanza akidai hana imani naye, ya pili yupo karibu na walalamikaji na mwisho alidai kwamba kesi yake aliomba kutosikilizwa na hakimu huyo ambaye alitoa hukumu ya kwenda jela miaka mitatu bila sababu ya msingi.

Kufuatia hali hiyo Hakimu Bi Kivelege alionekana kukasirishwa na barua hiyo,hivyo kumtaka mshitakiwa adhaminiwe upya na kumamuru Mkuu wa Kituo cha polisi kumweka mahabusu hali iliyowakasirisha ndugu zake na kuleta tafrani kubwa katika kituo hicho.

Hata hivyo baada ya kuona hali hiyo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi Inspekta Mwanga alimrejesha Bwana Laurence mahakamani ndipo zogo lililopoanza,hakimu akitaka dhamana ya awali ifutwe huku sababu za kufutwa hazikuwekwa bayana.

Wakati huohuo Hakimu hakuendelea na kesi huku akiondoka na gari yake akiacha kesi nyingine bila kusikilizwa lakini katika uchunguzi uliofanya ulibaini kuwa jumla ya kesi 9 zilizohukumiwa na hakimu huyo zimekatiwa rufaa kutokana na watuhumiwa kuachiwa huru mahakama ya wilaya hali inayotia shaka utendaji kazi wake.

Na. mdadisi wetu.
Hii ndiyo ratiba iliokuwa ikiongoza shughuli nzima ya kutoa heshima za mwisho za mpendwa Ms. Leocardia Rugimba, aliekuwa Mkurugenzi wa Vipindi Maaluu -TBC hadi umauti unamkuta.

Watu mbali mbali wakiendelea kutoa heshima za mwisho kwa Ms. Leocardia Rugimbana.



Ohoooo, ndivyo mama Ms. Leocardia Rugimbana aliekuwa Mkurugenzi wa Vipindi maalum TBC alivyozaliwa.


Mfanyakazi wa TBC Ms. Rose, akionekana ana huzuni sana juu ya kuondokewa na mpendwa Ms. Leocardia Rugimbana.

Mfanyakazi wa TBC ndugu F. Chilumba, akitafakari juu ya kuondokewa na mpendwa wetu Ms. Leocardia Rugimbana, ambambo alikuwa boss wake wa idara ya masoko kabla ya kubadilishiwa idara ya vipindi maalum hadi mauti ilipomkuta.
Hii ndio nyumba ya mwisho ya mpendwa wetu Ms. Leocardia Rugimbana, mama tutakukumbuka sana, maana wewe ulikuwa sii boss tu, ila ulikuwa ni kama mama.


Padri aliyeongoza misa ya kumuombea mpendwa wetu Ms. Leocardia Rugimbana, akijadili jambo na moja ya ndugu wa marehemu kabla ya mwili wa marehemu kuingia nyumbani kwake Tabata, Marehemu anatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kesho tarehe 28/7/12 kwa ajili ya mazaishi.


Baadhi ya wafanyakazi wa TBC, wakiwa na majonzi makubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao Ms. Leocardia Rugimbana, kwa kweli ni huzuni sana. Tutakukumbuka daima kwa ucheshi na upendo wako mama Leocardia.
Hivi ndivyo msiba ulivyokuwa, mpendwa wetu Ms. Leocardia Rugimbana ametutoka wana TBC, daima tutakukumbuka mama, tulikupenda sana ila mungu akakupenda zaidi, pumzika kwa amani mama. Amen.

Thursday, July 26, 2012

Katika Ukursa wake wa Facebook kaanza kuandika hivi:
DR. JOSE Chameleone


I AM VERY DISAPPOINTED!

I WAS HIRED BY GLOBAL PUBLISHERS A TANZANIAN COMPANY, TO PERFORM AT THE NATIONAL STADIUM ON THE 7th July 2012.

I PERFORMED AS THE CONTRACT AGREED! ON SUNDAY 8th ONE ERIC SHIGONGO THE CEO GLOBAL PUBLISHERS CONFISCATED MY PASSPORT ALLEGING MY MANAGER HAD SWINDLED HIS 3500$, WHICH IN REAL SENSE WAS SWINDLED BY A KAMPALA CONMAN CALLED GEORGE.

I WAS ASSISTED BY THE UGANDAN EMBASSY IN DAR EL SALAAM, WHO GAVE ME A TEMPORARY DOCUMENT TO RETURN ME HOME.
ON RETURN TO UGANDA I HUNTED FOR THE CONMAN, ARRESTED HIM AND HANDED HIM OVER TO POLICE, WHO FREED HIM ON CONDITIONS I DON'T KNOW!

I EXPLAINED TO THE TANZANIAN AMBASSADOR AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION IN UGANDA FOR ASSISTANCE BUT SEEMS IN VAIN.

I HAVE UPCOMING PERFORMANCES IN

SOUTH AFRICA, ENGLAND,BELGIUM, NORWAY,SWEDEN, CANADA ETC!

SO IS ERIC SHIGONGO ABOVE THE LAW TO KEEP MY PASSPORT ILLEGALY?

AM I LIABLE TO HIS NEGLEGANCE THAT HE TRUSTED A CONMAN?

IS IT FAIR THAT AN UNAUTHORIZED TANZANIAN CITZEN CAN KEEP MY PASSPORT FOR OVER A MONTH?

I NEED ADVICE


Akaendelea hivi:

ERIC SHIGONGO AM BOUND TO MAKE YOU AN EAST AFRICAN CELEBRITY GOR TAKING THE LAW THE WAY YOU WANT! WE ARE PLANNING EAST AFRICA UNION AND U ARE PROMOTING YOUR SELFISH UNION! Damn
Akaendelea tena:I AM AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION IN DEMOSTRATION FOR THE CONFISCATION OF MY PASSPORT BY A TANZANIAN ILLEGALY ERIC SHIGONGO I NEED MY FREEDOM TO TRAVEL AS A UGANDAN!

I NEED MY PASSPORT BACK ASAP!

FOR GOD AND MY COUNTRY UGANDA.NA TENA:
Woken up! AM NOT GOING TO GO BACK TO MY HOUSE! AM GOING TO SLEEP AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION UGANDA UNTIL MY BROTHER FROM TANZANIA SURRENDERS BACK MY PASSPORT TO UGANDA GOVERNMENT THAT OWNS IT.HE IS HOLDING IT ILLEGALLY- IF NO BODY IS THERE FOR MY RIGHT AND JUSTICE LET ME ASK FOR IT MYSELF!

I AM DEMONSTRATING AGAINST INJUSTICE
AND WANT ERIC SHIGONGO TO RESPECT MY COUNTRY!

FOR GOD AND MY COUNRTY I DECLARE
Mheshimiwa Dkt. Jakaya M. Kikwete akimkaribisha Ikulu Askofu Mkuu Protase Rugambwa.