MALAYSIA: HAWA NDIO MAPACHA WALIOTENGANISHWA.
Mara kadhaa watoto mapacha wanapozaliwa wakiwa wameungana huwa inakua kazi nzito kuwatenganisha na wakati mwingine huwa wanafariki wakiwa kwenye zoezi la kutenganishwa na wengine wanapoteza maisha kutokana na pesa ya hayo matibabu ya gharama kukosekana lakini kwa Malaysia wamepata bahati wakati huu.
Kuna watoto walizaliwa April 2011 wakiwa mapacha walioungana mguuni ambapo baada ya juhudi za Madaktari mabingwa kufanya upasuaji, wamefanikiwa kuwatenganisha hawa malaika Muaiman na Muaimin na wakabaki kuwa hai.
Idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wazazi waliokua wanaifatilia habari ya watoto hawa wamejawa na furaha baada ya kusikia hilo zoezi limefanikiwa.
Pamoja na kwamba upasuaji umefanikiwa, ugumu ulikuwepo kwenye sehemu ya kuhifadhia mkojo mwilini ambayo pia ilikua imeungana toka wamezaliwa, sasa hivi wapo chini ya uangalizi wa kitaalam mpaka hali yao itakapo ruhusu kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa mujibu wa Star news paper.
__________________________________________________________
Kwa hisani ya Millard.
No comments:
Post a Comment