TAHADHARI...!!
"NIMEAMBUKIZA UKIMWI MAELFU YA WATU JIJINI DAR"...JANE WA MWENGE...
Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la
baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza
maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote
usifute
hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi
nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata
sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya
kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda
mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili
msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono na
wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi
huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana
anayekupenda kiukweli sio uongo lazima asitake ngono kabla ya ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa
alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza na hata kulia mbele yangu
ili tufanye tu mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya
ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za starehe na mimi kwa sababu
ya upagani na kumwamini pia kwa sababu nampenda nilikubali tulienda
huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi ilikua
inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu akaagiza pombe alianza
kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi kunywa
pombe katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi
nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda
zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua
nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu maana
nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo nakunywa
mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu naonja ili
kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti
najua nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana nakumbuka
tulitoka pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na
kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba
maana tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi
kufanya mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono
na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar zote. Nilijikuta
natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia
maana alijua atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku hiyo lakini
kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo maana mwili
wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo
mpenzi wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana
tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo
sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu
wengine lakini sio kwangu alisema ”JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA
SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa
nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe,
kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia Arusha
huku akisema neno moja la mwisho kwamba ”shetani amemtuma kuwaambukiza
wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU nihurumie
mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao haukunistahili mimi. Hata leo hua
najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe na huyu
wakala wa shetani wamenifanyia hivi. Baada ya kujua nina UKIMWI na hali
hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume ambao
walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii
niliwakubali ili nami nife na wengi.
Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3
niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini
wakati huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga
na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua
kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao
wana UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500
maana ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu
niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi
wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la ”TUKO
WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa
nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku naombewa nilikutwa na mapepo mengi
sana na hata waombeaji wakashangaa. Ningejua ningeokoka tangu nikiwa
na miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa kubadirisha hali
hiyo.
Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni
dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila
kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi
kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana
kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV
hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua
kama uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda kanisani ukaombewe na kama una akili
mpe YESU maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe
maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo
wala sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi
sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia misibani
huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni
na waume zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa
au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye
UKIMWI ni wengi kuliko unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani/msikitini na pia soma BIBLIA/KURAAN na uwe mtakatifu/mcha mungu.
MUNGU akubariki.
Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
source KIBO MEDI GROUP - DAR.