Wednesday, October 31, 2012

TAHADHARI... Maandamano ya waislamu yazuiwa........!!


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limezuia maandamano ya baadhi ya Waislamu yaliyotangazwa kufanyika Novemba mosi na mbili mwaka huu ya kushinikiza kutolewa rumande kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa ma

andamano hayo ni batili kutokana na kutopewa baraka na jeshi hilo.

Alisema polisi imejipanga kuwashughulikia wote watakaofanya maandamano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi linamsaka mtu anayechapisha vipeperushi vya kuchochea maandamano ambayo ni hatari kwa wananchi.

Aliwataka wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi kutokana na kuimarishwa kwa usalama katika siku hizo ambazo watu hao wanataka kuandamana kinyume cha sheria.

“Hatutarudi nyuma kwa wale ambao watavunja sheria na kuvuruga amani ya nchi katika siku hizo mbili,” alisema Kova.

Kova alisema haki itapatikana mahakamani, hivyo hakuna haja ya kufanya maandamano katika mahakama hiyo ambayo inasikiliza kesi ya kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment