Saturday, October 19, 2013

INATISHA: 
HABARI PICHA - HALI ILIVYOKUWA KATIKA UVAMIZI WA DUKA KUBWA NCHINI KENYA









Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.

Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.

Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.

Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake.

Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao zakawaida.

No comments:

Post a Comment