Thursday, February 28, 2013

Monday, February 25, 2013

PIGO BAADA YA PAPA KUTANGAZA KUACHIA MADARAKA.

Padre mkuu wa kanisa katoliki,Uingereza ajiuzulu.


Saturday, February 23, 2013

SAMAKI WA AJABU, HII SIO GRAPHICS WAPENDWA, AMINI USIAMINI, NDUGU ZANGU MSIOKULA KITIMOTO NA HAPO JE, MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Thursday, February 21, 2013

MAENDELEO: KITAIFA
HONGERA MZEE KIBAKI, RAIS WA JAMHURI YA WATU WA KENYA, KWA KUZINDUA BARABARA IITWAYO "MWAI KIBAKI ROAD" HAPA TANZANIA LEO 21/02/2013, WAKENYA KARIBUNI SANA TANZANIA.




Wednesday, February 20, 2013

WAKATOLIKI DUNIANI KOTE .... NI NGUMU KUAMINI...!!!

HATIMAYE MAZIKO YA MPENDWA PADRI EVARIST  GABRIEL MUSHI YAFANYIKA LEO 20/02/2013 HUKO ZANZIBAR.

Mamia ya wananchi, Rais na viongozi mbali mbali wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania bara na zaidi ya maaskofu 10 wamehudhuria maziko ya Padri Eavarist G. Mushi, aliuawa kinyama kwa kupigwa Risasi siku ya Jumapili tarehe 17/02/2013 akiwa anaenda kuongoza ibada ya misa takatifu siku ya jumapili.

MUNGU AMETWAHA NA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.. Amen.









KIDATO CHA NNE - 2012 WAFELI 60%
Unadhani nini kimepelekea vijana wa Form 4 Kuchora Zombies, kuandika Matusi, mistari ya Hip-Hop na barua za mapenzi kwenye mitihani yao? Tumefikaje hapa?

Baada ya wananchi na wadau kupinga kwa nguvu suala la bunge kutorushwa LIVE kupitia televisheni, Bunge sasa limekuja na utaratibu mpya kabisa ambapo ofisi ya bunge ndiyo itakuwa na jukumu la kupiga picha ndani ya ukumbi wa bunge na kuzilisha TV zote zinazohitaji kurusha matangazo hayo...

Je una maoni gani kuhusiana na utaratibu huu? 

Monday, February 11, 2013

BREAKING NEWS...!!
KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI, POPE BENEDICT wa "xvi" AAMUA KUTANGAZA KUJIUZULU UPAPA KUANZIA TAREHE 28 February, 2013, ZAIDI YA MIAKA 600 HAIJAWAHI KUTOKEA PAPA KUJIUZULU.

MAELEZO:
POPE ANA MIAKA IPATAYO 85, NA KUJIUZULU KWAKE KUNATOKANA NA UMRI WAKE NA KUSHINDWA HATA KUTEMBEA SASA.






Monday, February 4, 2013


Ndege za kijeshi za Ufaransa, zimeshambulia kwa mabomu ngome za wapiganaji na maghala yao ya silaha katika maeneo ya vijijini ili kujaribu kukata njia wanazopitishia silaha zao.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius, waasi hao hawatweza kuendelea kupigana bila kupata chakula na silaha wanazohitaji.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa bei ya chakula na mafuta imepanda sana huku baadhi ya wafanya iashara wakitoroka kwa hofu ya kushambuliwa.Ndege 30 za kijeshi, zilifanya mashambulizi siku ya Jumapili, latika eneo la Tessalit huku kukiwa na hofu, kuwa wapiganaji hao huenda wakajipanga upya

Mkutano wa Kidal

Bwana Fabius alisema kuwa mashambulizi yaliyofanywa Jumapili, yalinuia kushambulia ngome za wapiganaji hao pamoja na vituo vya mafuta.



Askari wa Ufaransa nchini Mali

Alisema :''Ukitazama ramani, wameweza kujificha katika meeno ya Kaskazini. Lakini wanaweza kusalia huko kwa muda mrefu, ikiwa wana njia ya kupata bidhaa. Kwa hivyo, jeshi linajaribu kuziba kabisa njia za wao kupitishia bidhaa hizi.''
Lakini bwana Fabius hangeweza kusema ikiwa mashambulizi ya angani yananuia kuandaa majeshi kupigania ardhini.
Jeshi la Ufaransa, lilianza kusaidia jeshi la Mali kupambana na wapiganaji nchini Mali tarehe 11 January wakati wapiganaji wa kiisilamu walipoanza kuelekea Kusini mwa nchi na kutishia mji mkuu Bamako.
Tangu hapo, wapiganaji hao wamefurushwa kutoka maeneo ya raia Kaskazini na Mashariki mwa nchi.
Mji wa Kidal unasalia kuwa mji wa pekee muhimu ambao wanajeshi wa Ufaransa wangali kuukomboa kikamilifu.


Wapiganaji wa Kiislam nchini Mali

Mwandishi wa BBC nchini Mali amesema mashambulio hayo yamelenga maeneo ya milimani kaskazini mwa mji wa Kidal, ambako waasi hao wanadaiwa kujificha. Majeshi ya Ufaransa yamekuwa yakijaribu kuutwaa mji huo baada ya kuuteka uwanja wa ndege wa mji huo Jumatano.
Waasi wa kikundi cha Tuareg, ambao walikuwa wameudhibiti mji huo, wanaweza kuuachia kwa njia ya mazungumzo.
Askari wa Ufaransa wameudhibiti uwanja wa ndege wa Kidal.
Mashambulio hayo yanafuatia ziara ya Rais Francois Hollande wa Ufaransa nchini Mali Jumamosi.
Rais Hollande amesema majeshi yake yataendelea kuwepo nchini Mali hadi pale majeshi ya Afrika yatakapopelekwa kuilinda nchi hiyo.