Friday, October 26, 2012

Mwanafunzi anayeuza bikira yake kwenye mnada apata wanunuzi kibao.
Mwanafunzi anayeinadi bikira yake kwenye mnada kwa ajili ya mwanaume yeyote atakayetoa dau kubwa kuliko wote amepagawa na madau makubwa anayopewa, hivi sasa dau limefikia dola milioni 3.7

Natalie Dylan, 22, wa California nchini Marekani amesema hadi sasa wanaume 10,000 wameishajitokeza kuwania kuvunja bikira yake kwa kufanya naye mapenzi kwa usiku                mmoja tu.

Dylan ana mpango wa kutumia hela atakazopata baada ya kuuza bikira yake kulipia masomo yake ya shahada ya juu ya familia na ndoa.

Mwezi septemba wakati alipotangaza bikira yake kwenye mnada alipata dau la dola 243,000 lakini baada ya hapo dau lake limekuwa likiongezeka kwa kasi sana.

Hivi sasa mdau mmoja anayewania bikira ya binti huyo ametangaza dau la dola milioni 3.7.

Mwanafunzi huyo ambaye ana shahada ya masomo ya kinamama alisisitiza hakuwa akimaanisha kuwa anajiuza.

Dylan alisema ameamua kuvunja bikira yake na mwanaume atakayeshinda dau kubwa baada ya kuona dada yake Avia,23, ameweza kujilipia mwenyewe masomo yake baada ya kufanya ukahaba kwa muda wa wiki tatu tu.

Dylan alisema yuko tayari kwenda hospitali kupimwa bikira yake kama mdau yoyote atakuwa na mashaka na bikira yake.

"Nimepata wadau wengi wanaotaka uchumba lakini nimeweka wazi kwamba sitafuti mchumba na hii ni kwaajili ya usiku mmoja tu " alisema Dylan.

"Najua watu wengi watalaani kitendo changu kwakuwa si cha kawaida lakini mimi sitajali watakachosema " aliongeza Dylan.

No comments:

Post a Comment