Sunday, March 10, 2013

BONGE LA STUDIO - IN UK

KENYA  BROADCASTING CORPORATION - KBC, MKO JUUU.

UCHAGUZI KENYA: Uhuru Kenyatta ashinda kiti cha Urais!


Baada ya matokeo ya majimbo yote 291 kuripotiwa, Uhuru Kenyatta amejinyakulia jumla ya kura 6,173,433 sawa na 50.03% ya kura zote, huku Raila Odinga akichukua nafasi ya pili na jumla ya kura 5,340,546, sawa na 43.28% ya kura zote. Jumla ya kura zilizopigwa ni 12,338,667.

TUNAMPONGEZA UHURU KENYATTA kwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kenya.

Friday, March 8, 2013

MAJONZI MAKUBWA - DUNIANI.
Hugo Chavez hakupendwa na kila mtu Venezuela wakati wa utawala wake.Wapinzani wa Hugo Chavez wakisherehekea katika moja ya kumbi za maburudiko baada ya kupokea habari za kifo chake mjini Florida, Marekani
Maelfu walijitokeza kuomboleza na kuusindikiza mwili wa Chavez katika moja ya kumbi zinazosemekana kuwa kumbukumbu za waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini 
Mwili wa Chavez umelazwa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi mjini Caracas na marais wa nchi jirani walifika kutoa heshima zao za mwisho akiwemo Rais wa Bolivia Evo Morales na mwenzake wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner.
Chavez alikuwa na maadui wengi pamoja na wale waliomuona kama mwokozi wao kwa sababu ya sera zake za kisosholisti.
Mwili wa Chavez ulipitishwa katikati ya mji mkuu Caracas na kusindikizwa na maelfu ya watu waliomuunga mkono 
Chavez alionekana kama mpigania haki za watu maskini kwa kusisitiza sera zake za kisosholisti na kuzichanganya na demokrasia. 
Mwaka 2011 Chavez alisema kuwa anapokea matibabu ya Saratani nchini Cuba
Mwaka uliofuata Chavez alichaguliwa na wananchi kuongoza kwa muhula wwingine wa miaka sita kuiongoza Venezuela
Kifo chake kilitangazwa na serikali ya Venezuela Jumanne wiki hii Mwili wa marehemu Rais wa Venezuela Hugo Chavez umepitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.


"Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao"

SIASA - KENYA: 
KIVUMBI CHA URAIS 2013 BADO HALI NI TETE, HUENDA "RAIS EMILIO MWAI KIBAKI" AKAENDELEA NA WADHIFA WAKE MPAKA MWEZI WA TANO (5) 2013, KUSUBIRI UCHAGUZI MPYA, HII NI SABABU YA 5% YA WAPIGA KURA WOTE KUHARIBIKA. KILA LA KHERI WAKENYA.



Saturday, March 2, 2013

JARIBU KUKUMBUKA

UKATILI WA KUPINDUKIA




Nasra Mohammed (38) - Alieuawa kwa kuburuzwa na gari na mumewe.

Mkazi wa Bunda mkoani Mara, Elisha Makumbati anadaiwa kumfanyia ukatili wa kupindukia mkewe, Nasra Mohammed (38) kwa kumburuza na gari uvunguni, umbali wa mita 150 baada ya kutokea kutoelewana kufuatia wivu wa kimapenzi.
Akizungumza, dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwanne Daudi, ambaye alishuhudia tukio hilo alisema:
“Mdogo wangu alifanyiwa ukatili wa kutisha na mumewe kwani Februari 2, mwaka huu mimi na Nasra tulikuwa tunatoka kwenye saluni moja iliyopo mtaa wa Posta, maeneo ya Bunda.
“Tukiwa njiani ghafla tulimuona Elisha ambaye ni mumewe akiwa kwenye gari aina ya Nissan Patrol lenye namba za usajili T 400 BBC na kulisimamisha mbele yetu kisha akamuita mdogo wangu kwa hasira.
“Nasra alivyoenda akamuuliza mumewe, kwa nini alitaka kuwagonga, wakaanza kulumbana na kushutumiana kwa wivu wa kimapenzi,” alisema Mwanne.
Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema huku akitokwa na machozi: “Baada ya kumaliza malumbano yao mimi na Nasra tulianza kuondoka, ghafla tukashtukia mumewe akiondoa gari kwa kasi na kumgonga mkewe na kumburuza kwa umbali wa mita 150 kwa mujibu wa kipimo cha jeshi la polisi lililopima ajali hiyo.
“Wakati akimburuza mdogo wangu mimi na umati uliokuwa ukishuhudia tulipiga mayowe ya kumtaka Elisha asimamishe gari lakini aliendelea kuongeza mwendo huku damu zikitapakaa barabarani mpaka alipokwenda kukutana na tuta ndipo mwili ukachomoka uvunguni mwa gari.
“Mdogo wangu Nasra wakati akisagika kwenye lami mimi nilikuwa nikilikimbiza gari hilo kwa nyuma. Nilipofika eneo alilochomoka nilimkuta askari wa usalama barabarani ameshafika na tayari alianza kupima ajali hiyo na muda si mrefu lilifika gari la polisi ‘Difenda’ na kumpakia Nasra na kumpeleka Hospitali ya Bunda, maarufu kama DDH.
“Alipopimwa aligundulika amevunjika mbavu saba zilizosababisha kutoboa mapafu, mguu wa kushoto na kupata majeraha makubwa mgongoni na sikio la kushoto lilikuwa limenyofoka, kutokana na hali hiyo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza na kufikishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Dada huyo wa marehemu alizidi kusema: “Hali ya mdogo wangu iliendelea kuwa mbaya ambapo Juni 16, mwaka huu, Hospitali ya Bugando ilimpa uhamisho wa kwenda Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) 
“Akiwa Muhimbili madaktari walimtoa nyama za sehemu mbalimbali na kumrudishia mgongoni baada ya kuona nyama yote ya mgongoni zilitoka na kujikusanya sehemu ya makalioni.
“Marehemu mdogo wangu aliendelea kuugulia maumivu ambapo Jumanne iliyopita, saa saba za usiku aliaga dunia na tumemzika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar,” alisema Mwanne huku akifuta machozi na akadai mtuhumiwa mpaka sasa yupo huru mitaani.
Juhudi za gazeti hili kuzungumza na mtuhumiwa huyo ziligonga mwamba baada ya simu zake za mkononi kutopatikana hewani. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya amelaani kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi nchini kumkamata mtuhumiwa huyo.


End..!